Nnape Nnauye fundi wa mpila alijisahau kucheza kwa maelezo ya kocha wake


Nnape Nnauye fundi wa mpila alijisahau kufuata maelekezo ya kocha wake
Tokeo la picha la nnape, makonda na magufuli picha

Muundo wa serikali yoyote rais ndiye mwajibikaji wa kwanza kwa chochote kitakachofanyika na uongozi wa serikali yake,kama kocha atakavyohusishwa na matokeo mabovu au mazuri ya team yake
Rais ndiye atakayelaumiwa au atakayesifiwa na ndiyo maana sasahiv rais amekuwa akilaumiwa saana katika dhana ya kutomwajibisha mkuu wa mkoa dar es salaam Mh. Paul Makonda

licha ya kucheza vizuri kwa aliyekuwa waziri wa michezo mh Nnape Nnauye lakini bado alikuwa hachezi kwa maelekezo ya kocha wake aliyempa nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi
Nnape nikama alikuwa hajui kocha wake anataka nini, ama aliamua kucheza anavyojisikia yeye, na nikatika dhana hiyo ndipo utakapomuona makonda anacheza rafu nyingi na usimpende lakini ni katika rafu hizo makocha kama mourinho wanaamini watapata matokeo na wanahitaji mchezaji wao acheze, hata magufuli anamwamini makonda kama mchezaji wake mwenye nidhamu na anayekamilisha majukumu aliyopangiwa uwanjani

kwa hali hiyo sisi mashabiki tunaumia sana kumtoa uwanjani fundi wetu , pasina kujiuliza mara mbili kwanini kocha anamtoa
inatuuma tunapomwona akiwa na ufundi mwingi lakini amewekwa benchi

Hakika Nnape alikuwa kiongozi mzuri lakini mimi na wewe hatujui magufuli ana malengo gani ya kukamilisha sasahiv
Anatuongoza lakini hatujui dira yake na malengo yake ya miaka mitano na ndiyo sababu hatuwezi kujua yupi angemfaa kufikia malengo kama yeye anavyofahamu wakumfaa na kuingia kwenye team yake

nipe usauri wako  hapo chini


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAKWIMU - Epl ligi bora duniani ikifuatiwa na la liga